Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Monday 15 April 2024

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA 13 WA KAUKI

Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya Wanaukoo Wote; wanayofuraha kubwa kuwakumbusha kuwa Mkutano Mkuu wa 13 wa KAUKI unatarajia kufanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Juni 2024, Kijijini Kidamali, Mkoa wa Iringa. Mkutano huu ni Mwendelezo wa Mikutano ya Ukoo ambayo hufanyika kila Mwaka. 

Ili kufanikisha Mkutano huo, Wanaukoo Wote wanaombwa kutoa Michango yao ili kufanikisha Mkutano huo. Watu Wazima Watachangia Shilingi 10,000/- na Watoto 5,000/-. Michango hii itasaidia upatikanaji wa huduma za Chakula, Chai na Maji kwa Siku zote tutakazokuwa Kidamali. Michango itolewe kwa Viongozi wa Kanda Husika. 

Malengo ya Mkutano Mkuu ni pamoja na:

1. Kutambulishana na Kufahamiana Ndugu/Wanaukoo;

2. Kujua Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;

3. Kubadilishana Taarifa na Uzoefu Mbalimbali wa Shughuli za Maisha;

4. Kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha undugu na ushirikiano baina ya Wanaukoo; na mengineyo.

Mikutano ya KAUKI huhudhuriwa na Wanaukoo kutoka Maeneo ya Magubike, Kidamali, Kalenga, Nzihi, Nyamihuu, Nyamahana, Nduli, Mgongo, Itagutwa, Igominyi, Vilalo, Migoli, Iringa Mjini, Mafinga, Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza na Maeneo mengine ambayo washiriki wanaishi.

Imeandaliwa na Kutolewa na:


Viongozi wa KAUKI

Sambaza kwa Ndugu Wote.

Thursday 21 September 2023

NGOMA ZETU WAKATI WAHUZUNI

Bing Videos


https://www.bing.com/videos/riverview/relatedvideo?&q=Wahehe+Songs&&mid=47079E551DF28755881447079E551DF287558814&&FORM=VRDGAR 

Tuesday 12 September 2023

MIKUTANO YA KANDA YA KAUKI



Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) ulifanya Mkutano wa DHARURA siku ya Alhamisi ya Tarehe 7 Septemba 2023 Kijijini Kidamali kwa Lengo la kuhimiza Wanaukoo wa Kivenule kuendelea kufanya Mikutano ya UKOO. Mkutano huo wa dharura uliofanyika baada ya mazishi ya Marehemu Stewart Edgar Kivenule.

Pamoja na Mambo mengine, Wanaukoo walipendekeza Tarehe ya Mkutano Mkuu wa Ukoo ambao utafanyika Tarehe 29 Juni 2024, Kijijini Kidamali, Mkoani Iringa.

Aidha Viongozi wa Kanda mbalimbali waliombwa kufanya Mikutano ya UKOO ya Kanda ili kuweka mikakati ya kuweza kufanikisha Mkutano huo.

Ikiwa ni Pamoja na kusambaza taarifa na kuweka taratibu za michango kwa ajili ya kufanikisha Mkutano huo.

Imeandaliwa na Umoja wa UKOO wa Kivenule (KAUKI)

Sunday 10 September 2023

TANZIA

 


Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya Familia ya Edgar Sigatambule Kivenule wa Kibamba, Dar es Salaam, wanatangaza kifo cha ndugu yetu Stewart Edgar Kivenule kilichotokea Mkoani Dodoma, usiku wa kuamkia tarehe 04 Septemba 2023 kwa ajali ya gari.

Mazishi ya Marehemu Stewart Edgar Kivenule yamefanyika Kijijini Kidamali, Mkoani Iringa tarehe 7 Septemba 2023.

Ukoo wa Kivenule unawapa pole ndugu, jamaa na marafiki ya Familia ya Edgar Kivenule na Steward Kivenule.

Mungu Aiweke Roho yake Mahali Pema Peponi, Amina.



TAARIFA MUHIMU KWA WANAUKOO WA KIVENULE

Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) ulifanya kikao cha dharura cha masaa matatu (3) tarehe 7 Septemba 2023 siku ya Alhamisi, Kijijini Kidamali baada ya kuhitimisha mazishi ya ndugu yetu Steward Edgar Kivenule.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa UKOO wa Kivenule Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule; na kilihudhuriwa na Wanaukoo wengi waliohudhuria mazishi ya Marehemu Stewart Edgar Kivenule.

Agenda Kuu ya Kikao hicho ilikuwa ni kujadili changamoto zilizosababisha kutoendelea kufanyika kwa Mikutano ya UKOO. (Taarifa Rasmi itatolewa).

Aidha UKOO wa Kivenule kupitia Mkutano huu umeazimia kwa Pamoja kuendelea kufanya Mikutano ya UKOO wa Kivenule.

Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ujao umepangwa kufanyika Tarehe 29 ya Juni 2024 Kijijini Kidamali. Lengo la kufanyika Kidamali ni kuendelea kuongeza hamasa kwa Wanaukoo wote, na hasa ikizingatiwa kuwa Kidamali kuna mkusanyiko mkubwa wa ndugu.

Kabla ya kufanyika kwa Mkutano huo, kutakuwa na Vikao vya Utangulizi kwa Viongozi wa Kanda mbalimbali ili kuweza kuwasilisha taarifa na pia kuweka mikakati ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Mwaka 2024.

Imetolewa na Uongozi wa KAUKI